Rais wa Uganda Yuweri Museveni ameamuru kusitishwa kwa mfuko wa mamilioni ya fedha ulioanzishwa na nchi wahisani, baada ya kutoa malalamiko kwamba mfuko huo wa fedha unaendeshwa na wageni na wanaodhoofisha uhuru wa taifa la Uganda.
Katika barua yake bwana Museveni amewatakapolisikuchunguza namnawizara ya fedha nchini humo ilivyowaruhusu wafadhilikutoka mataifa ya kigeni bila ya kupata idhini ya serikali
Kituo cha Utawala wa demokrasianchini humo kinafadhiliwa na wafadhili saba, ikiwekoJumuiya ya umoja waUlaya.
Lakini Kusimamishwa kwa mfuko huo wa fedhakunaweza kuwa na athari kubwa nchini humo kwani unasaidia kufadhili mashirika mengi yanayokua nayanalengahaswa demokrasia na haki za binadamu.
Bw Museveni alishinda uchaguzi wa urais mwezi uliopita jambo linalofanya kuwa madarakani kwa muhula wa sita sasa lakini Mpinzani wake mkuu Bobi Wine alisema kuwa uchaguzi huo uligubikwa na udanganyifu mkubwa japo Museveni amesema kuwa uchaguzi huo ndio ulikuwa wa haki na wa wazi kuwahi kushuhudiwa nchini Uganda.