LEO FEBRUARI 1,2021 MAADHIMISHO YA SIKU YA SHERIA DODOMA.

“Jaji Mkuu hapa umezungumza kiswahili kizuri kuliko changu cha kisukuma, lakini ukienda kuhukumu unaandika kingereza, hicho kiswahili kinapotelea wapi? hii ni changamoto kubwa, lazima tubadilike na tukipende chetu.


Ukimuandikia hukumu mtu kule Kijiji katahoka, Biharamulo kwa kingereza yule bibi kizee aende akatafute wa kutafsiri?. Tunatengeneza kero kwa wananchi, kuandika hukumu kwa kiswahili sio dhambi.” Rais Magufuli.

“Sasa wakati umefika wa kuanza kuweka mikakati ya lugha ya kiswahili kutumika kwenye masuala ya kimahakama na sheria katika ngazi zote. Kiswahili kinatumika AU, SADC, EAC , sioni sababu ya kwanini Mahakama hamtaki kutumia kiswahili.” Rais Magufuli.

“Nimekaa miaka mitatu UDSM nikisoma masomo yangu ya Sayansi, Chemistry na Mathematics vyote vinaandikwa kwa kingereza, nimefanya PHD, nimekaa Uingereza mwaka mzima bado wanasema sijui kingereza, sijui nilikua nazungumza kisukuma kule. Niliamua kuzungumza Kiswahili kukidumisha kwa sababu ni lugha iliyoachwa na Baba wa Taifa.” Rais Magufuli.