Baraza la Mitihani nchini (Necta) limetangaza matokeo ya kitaifa ya upimaji wa maarifa kwa darasa la nne, kidato cha pili na kidato cha nne kwa mitihani iliyofanyika mwaka jana, 2020.
Akitangaza matokeo hayo jijini Dar es Salaam, leo (Ijumaa), Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, Dk Charles Msonde amesema ufaulu umeongezeka kwa asilimia 3.09 ikilinganishwa na yale ya kidato cha nne kwa mwaka 2019.