Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa leo ametembelea katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam na kukagua maandalizi ya tukio la kuagwa kwa mwili wa Hayati Dkt. John Magufuli, litakalofanyika Jumamosi Machi 20 na Jumapili, Machi 21, 2021.

Mhe. Majaliwa amesema ameridhishwa na maandalizi yanayofanywa chini ya usimamizi wa Kamati ya Kitaifa ya Maafa ambayo yeye mwenyewe ndiye Mwenyekiti wake akishirikiana na Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Hemed Suleiman Abdulla.
You must be logged in to post a comment.