
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema kuwa Miwili wa aliyekuwa Rais Dr John Pombe Magufuli utazikwa Machi 25 mwaka huu nyumbani kwake Chato, mkoani Geita.
Ameeleza hayo wakati alipohutubia taifa punde baada ya kuapishwa Ikulu Dar es salaam
Rais Samia amesema kuwa kesho Machi 20, 2021 mwili wa Hayati Rais Dk John Magufuli utatolewa Hospitali ya Jeshi Lugalo na kupelekwa Kanisa la St Peter’s Oysterbay, Dar es Salaam kwa Ibada na baadaye utapelekwa Uwanja wa Uhuru kuagwa na viongozi.
Machi 21,2021, wananchi wa Dar es salaam watapata fursa ya kumuaga mpendwa wao
Dk Magufuli na baadaye utasafirishwa kuelekea Dodoma.
Machi 22, wananchi wataaga mwili wa Rais Magufuli na kisha utapelekwa jijini Mwanza ambapo Machi 23, utaagwa Mwanza na kisha baadaye kusafirishwa kwenda Chato mkoani Geita.
Rais Samia Machi 24, Mwili wa Hayati, Dk John Pombe Magufuli utaagwa na wanafamilia pamoja na wananchi wa Chato, na Machi 25, Hayati Magufuli atafanyiwa maombi katika Kanisa Katoliki Chato na kisha kufuatiwa shughuli ya maziko.
You must be logged in to post a comment.