Klabu ya Dar Young African Imepata Kocha Bora atangaaza vita kwa Mtani

Kamati ya Ufundi ya Timu ya Dar Young African Imemchagua Hubert Velud Kuwa kocha Mkuu wa Klabu hiyo inayoshikiria nambari moja kwenye Ligi Kuu ikiwa tayari imepoteza matumaini ya kutwaa Kombe hilo baada ya kuwa na mwendelezo wa kufanya vibaya

Hubert Velud

Hubert Velud ni Kocha mzoefu kwa Bara la Afrika ambaye amewahi kuzifundisha vilabu vya ES Setif, US Alger, JS Kabylie na CS Constantine za Algeria, TP Mazembe ya DR Congo, Hassania Agadir na Difaa El Jajida za Morocco

Velud ambaye kwa sasa ni kocha wa timu ya Taifa ya Sudan amekubaliana kila kitu na uongozi wa klabu ya Yanga na atajiunga na klabu hiyo mwisho wa msimu huu (July) ili kuanza maandalizi ya msimu ujao. Kocha huyo atakuwa analipwa mshahara wa dola 20,000 kwa mwezi (Milioni 46.3 za Kitanzania).