Waziri Mkuu Awahakikishia Watanzania Hari ya Ukimya Rais Magufuli ni Mzima Wa Afya

Serikali ya Tanzania imeweka bayana kwamba Rais John Magufuli yu mzima bukheri wa afya hivyo Watanzania wapuuze taarifa zinazoendelea kusambazwa katika mitandao ya kijamii na kwamba wale wanaoendelea kuzusha hayo lengo lao ni chuki na kuzua taharuki miongoni mwa wanajamii.

Taarifa ya Serikali imetolewa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa baada ya Swala ya Ijumaa huku akikemea tabia ya baadhi ya Watanzania wanaoishi nje ya nchi kupotosha kwa makusudi mambo mbalimbali yanayohusu maendeleo ya nchi pamoja na kuzusha uongo.