Tanzania ‘kuchunguza wizi wa kikombe cha Ekaristi’. Kikombe cha Ekaristi Takatifu kutoka kanisa moja la katoliki nchini Tanzania kimeibiwa, kwa mujibu wa gazeti la Mwananchi.

Polisi bado wanachunguza jinsi kikombe hicho kilivyotoweka kutoka kanisani. Polisi bado wanachunguza jinsi kikombe hicho kilivyotoweka kutoka kanisani

Kikombe cha Ekaristi Takatifu kutoka kanisa moja la katoliki nchini Tanzania kimeibiwa, kwa mujibu wa gazeti la Mwananchi.

Wizi wa kikombe hicho cha Ekaristi kilicho na thamani ya dola 2,150 ulitokea Jumapili iliyopita katika Parokia ya Mkoka, iliyopo mji Mkuu wa Dodoma.

Polisi wanachunguza jinsi kikombe hicho kilivyotoweka katika majengo ya kanisa.

Aidha hakuna kitu kingine kilichoibiwa kutoka kanisani humo.

Na mpaka sasa hakuna mtu yeyote aliyekamatwa kutokana na wizi huo, gazeti hilo limemnukuu mkuu wa usalama wa eneo hilo.