Mtakatifu Francisca Wa Roma, Mtawa.
Mtakatifu Francisca alizaliwa mwaka 1384, huko Roma. Alizaliwa katika familia yenye uwezo na kuheshimika.
Akiwa umri wa miaka 11 alitaka kuwa mtawa, lakini alipofika umri wa miaka 12, aliozeshwa kwa Lorenzo Ponziani, ambaye alikuwa kamanda katika jeshi la Papa.
Ndoa yake ilikuwa nzuri, na alitumia muda ambao aliupata kwenda kuwatembelea maskini na wagonjwa, akiwasaidia kwa kila alichoweza. Alifuatana na wifi yake aliyeitwa Vannozza. Kuna nyakati za mafuriko na ukame, aliigeuza nyumba ya familia kuwa hospitali na kituo cha msaada.
Mwaka 1425, tarehe 15 Agosti, Mtakatifu Francisca, alianzisha shirika la watawa wa kike (The Olivetan Oblates of Mary ), na mwezi Machi 1433 alianzisha Manosteri huko Tor de Specchi, karibu na mji wa Campidoglio. Tarehe 4 Juni 1433, alipata kibali cha Papa Eugene IV.
Mtakatifu Francisca alibaki nyumbani kwake akimuuguza mumewe ambaye alikuwa mgonjwa. Mume wake alikufa mwaka 1436, na Mtakatifu Francisca alienda kuishi katika manosteri na kuwa kiongozi.
Mtakatifu Francisca alikufa mwaka 1440 Machi 9 na kuzikwa huko Santa Maria Nova, Roma. Mwaka 1608, alitangazwa mtakatifu na Papa Paul V.
*Watakatifu wengine wa leo ni:*
Mt. Anthony
Mt. Bosa wa York
Mt. Catherine wa Bologna
Mt. Pacian
Mtakatifu Francisca Na Watakatifu Wote Wa Mungu, Mtuombee!!…..🙏🏼