Rais wa CAF Ahmad Ahmad kuachia Madaraka Baada ya Rufaa yake Kutupiliwa mbali na Mahakama ya CAS

Motsepe

Patrice Motsepe anatarajiwa kuwa Rais wa Shirikisho la Soka Barani Afrika (Caf) wiki hii, baada ya baada mahakama ya kusuluhisha migogoro ya michezo (Cas) hii leo kupunguza adhabu ya marufuku ya kujihusisha na mpira kwa rais wa zamani wa Caf Ahmad Ahmad kutoka miaka mitano hadi miwili.

Safari ya bilionea huyo raia wa Afrika Kusini kuchukua hatamu ya uongozi wa Caf ilinyooka mwishoni mwa juma baada ya washindani wake watatu – Jacques Anouma, Augustin Senghor na Ahmed Yahya – kujiondoa kwenye kinyang’anyiro hicho. 

Kigingi cha mwisho kwa Motsepe, 59, kutawazwa siku ya Ijumaa ilikuwa uwezekano wa Ahmad kurejea ulingoni, endapo mahakama ingemuondolea kabisha marufuku inayomkabili.