Msemaji mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi amesema Serikali ya Tanzania na Kenya zinaendelea na mazungumzo ili kufahamu kiini cha kuzuiwa kwa Shehena ya Mahindi kutoka Tanzania kuingia nchini Kenya yakiwa kwenye magari eneo la Namanga Arusha pamoja na Holili na Tarakea Kilimanjaro mpakani mwa Tanzania na Kenya lakini katika maeneo mengine ya mpakani ukiwemo mpaka wa Horohoro Tanga hakuna zuio hilo.
Kwa maoni yako unadhani hatua iliyochukuliwa na nchi hiyo jirani ni sahihi hususani kwa bidhaa ambayo ilishazoeleka kuingizwa nchini humo kwa miongo kadhaa au nini kingefanyika kama suluhu?
Azamtv