PROF. MUSERU : Hospitali ya Taifa Muhimbili imefunga mashine nne Kujifukiza

Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Prof. Lawrence Museru amesema wamefunga mashine hizo ili kuunga mkono jitihada za Serikali katika kukabiliana na magonjwa yanayohusiana na mfumo wa upumuaji.

Hospitali ya Taifa Muhimbili imefunga mashine nne (Tatu Upanga na moja Mloganzila) za kujifukiza ambazo zimetengenezwa na SIDO ili kusaidia wagonjwa kupata tiba ya mfumo wa upumuaji kwa kutumia dawa za tiba asili zilizoidhinishwa na Serikali, gharama ya kujifukiza ni Tsh.Elfu tano kwa nusu saa.

“Wizara ya Afya ilielekeza kuimarishwa matumizi ya dawa za tiba asili kwa wagonjwa Hospitalini kama nyongeza kwenye tiba za kibingwa, Muhimbili imekuja na utaratibu wa kuwaruhusu wagonjwa kwa hiari yao kutumia dawa za tiba asili za kunywa na mvuke zilizoidhinishwa”

“Katika Hospitali zetu za Upanga na Mloganzila tuna Madaktari wa aina mbalimbali takribani 400, baadhi yao kupitia matumizi ya huduma hii ya tiba mvuke watafanya utafiti na kuwa katika nafasi ya kutuambia kama tiba hizi zinasaidia kwa kiasi gani”

“Ugonjwa huu wa Covid 19 ni mpya hakuna aliye na majibu sahihi, kwa hiyo ni muhimu kwamba hizi njia zinazojitokeza za kupambana na matatizo haya sisi tuliopo hapa tusizipuuzie bali tuzifanyie utafiti na kutoa majibu”