Meya wa Jiji la Dar es salaam Mhe. Omary Kumbilamoto ametimiza ahadi yake ya kukabidhi Kiti Mwendo (Wheelchair) kwa Mtoto Mwenye ulemavu Ally Amiri Mkazi wa Mtaa wa Mfaume Kata ya Liwiti.




Hafla hiyo ya Makabidhiano ya Kiti Mwendo (Wheelchair) yamefanyika nyumbani kwa Mama wa Mtoto huyo Bi Sophia Rashidi anayeishi Mtaa wa Mfaume Kata ya Liwiti.
Mhe. Kumbilamoto ameahidi kumsaidia Mtoto wa Bi Hadija Ramadhani ambaye amewasilisha maombi kwaajili ya Mjukuu wake Yahaya Bakari Mkazi wa Liwiti Mtaa Mfaume kwaajili ya kupatiwa Kiti Mwendo (wheelchair). Sambamba na hilo Mhe. Kumbilamoto ametoa ahadi ya kumkatia Bima ya Afya ya mwaka mzima Mtoto Ally Amiri ambaye maradhi yamekuwa yakimsumbua kwa muda mrefu.
Mhe. Kumbilamoto ameendelea kwa kumpongeza Diwani wa Kata ya Liwiti Mhe. Alice Mwangomo kwa hatua alizo zichukua kutoa taarifa za watoto hao ili waweze kusaidia. Lakini pia amempongeza kwa namna ambavyo anapambania maendeleo ya Kata Liwiti.
Lakini Mhe. Kumbilamoto amewataka Maafisa Ustawi wa Jamii ngazi ya Kata kushuka chini kwa Wananchi na kutoa taarifa hasa kwa watoto wenye uhitaji maalum ili waweze kusaidiwa kwani wengi wamekuwa majumbani na kukosa haki zao za Msingi ikiwemo kupata Elimu.
Mwisho Mhe. Kumbilamoto ameahidi kurudi baada ya wiki moja kwaajili ya kukabidhi Mabati 30, Mifuko ya Saruji kwajili ya ukarabati wa Madarasa ya Shule ya Msingi Liwiti. Lakini pia atakabidhi Kiti Mwendo kwa Mtoto mwengine mwenyewe ulemavu anayeitwa Yahaya Bakari.
Na Juma Mizungu, PuguMedia Online.
Jana Feb 27,2021.
You must be logged in to post a comment.