ACT Wazalendo Tayari Tumependekeza jina la Mrithi wa Maalim Seif Kwa Rais wa Zanzibar

Kiongozi wa ACT Wazalendo Zitto Kabwe amesema tayari Chama hicho kimeshapendekeza jina kwa Rais wa Zanzibar la Mtu ambaye atarithi majukumu ambayo Maalim Seif alikuwa anayafanya ya Umakamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, ametoa kauli hiyo kwenye hitma ya kumuombea Maalim Seif, DSM.

“Bahati nzuri, Maalim alikuwa ni Kiongozi, alijua kuna siku Mwenyezi Mungu atamchukua kwasababu sisi sote lazima turejee kwa Mwenyezi Mungu kama tulivyoambiwa na mafunzo ya Dini yetu na Dini zote, aliacha ametupa maelekezo ya nini kitokee iwapo atatangulia mbele ya haki”- Zitto

“Namshukuru Mwenyezi Mungu kwamba Viongozi wa Chama cha ACT wamefuata yale maelekezo yaliyoachwa na Maalim Seif kwa namna ambayo Kiongozi wetu alituelekeza (jina la Mrithi wa Maalim aliyependekezwa) na sasa umebaki wajibu wa Rais wa Zanzibar wa kuyatekeleza hayo”