Rais Magufuli leo amemuapisha aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM, Dr.Bashiru Ally kuwa Balozi na Katibu Mkuu Kiongozi akichukua nafasi ya Balozi Kijazi aliyefariki katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam leo tarehe 27 Februari 2021.

“Nakushukuru sana Rais Magufuli kwa imani yako kubwa kwangu, hii ni mara ya pili ukinipa imani ya kulitumikia Taifa letu katika wadhifa mkubwa kwanza ndani ya CCM na sasa hivi katika utendaji wa Serikali, imani hiyo nitailipa kwa imani”
“Rais Magufuli leo siwezi kusema mengi kwasababu ya mazingira niliyopata uteuzi huu, ulinipa kazi ambazo kwa ratiba zingeweza kuchukua Mwezi mzima wa tatu na tukaagana na ilikuwa niondoke kesho au keshokutwa, jana napata taarifa mtandaoni kuwa umeniteua”
“Mshtuko nilioupata (baada ya uteuzi) hauniwezeshi kusema mengi, bado natafakari nitafanya nini kukidhi matarajio yako Rais Magufuli kwa imani uliyonipa kwa mfululizo, Watanzania wote mniombee niweze kukidhi matarajio ya Rais Magufuli”- Balozi Dr.Bashiru
You must be logged in to post a comment.