KISINDA HANA NAMBA SIMBA. Msemaji wa Mabingwa wa Tanzania {SIMBA SC} Amemwambia Wachezaji wa Yanga kuwa ana Namba katika kikosi cha Simba ikiwa Ni mfululuzi wa Timu ya Wekundu wa Msimbazi ikiendelea Kufanya Vizuri kwenye Ligi ya ndani Vodacom na Ligi ya Klabu bingwa Barani Afrika

Msemaji wa Mabingwa wa Tanzania {SIMBA SC} Amemwambia Wachezaji wa Yanga kuwa ana Namba katika kikosi cha Simba ikiwa Ni mfululuzi wa Timu ya Wekundu wa Msimbazi ikiendelea Kufanya Vizuri kwenye Ligi ya ndani Vodacom na Ligi ya Klabu bingwa Barani Afrika



Licha ya kuwa sababu ya penati kwenye mchezo wa Ligi Kuu uliowakutanisha Yanga na Simba, Uwanja wa Mkapa, Tuisila Kisinda ameambiwa hawezi kupata namba ndani ya Simba.

Manara ameongeza kuwa anaamini kuwa kwa namna ambavyo anafanya ndani ya uwanja akiwa mwanariadha kama ilivyo kwa Filbert Bayi anaweza kutusua.
:
“Unazungumza kuhusu Kisinda,(Tuisila) kuja kucheza Simba? Sasa pale atacheza nafasi ya nani maana kila mtu ana namba yake sijui atamchomoa nani kikosi cha kwanza.
:
“Labda atapendeza akiwa kwenye masuala ya riadha kama akina Bayi,(Filbert) huko anaweza kufanya vizuri ila ndani ya Simba hakuna nafasi kwa kweli na huo ni ukweli kabisa.
:
“Unapozungumzia Simba unazungumzia timu moja ambayo kupata namba lazima ukomae na uwe bora ndani ya uwanja sasa na wachezaji ambao wanasajiliwa ni lazima wawe imara na bora,” amesema.