De Agosto Kuwakosa Wachezaji Saba Kwenye Mchezo wa Marudiano dhidi ya Namungo

Klabu ya Primiero de Agosto ya Angola 🇦🇴itawakosa wachezaji saba kwenye mchezo wao wa marudiano wa Kombe la Shirikisho barani Afrika dhidi ya Namungo FC 🇹🇿 kati yao ni pamoja na kiungo wa Kongo, Bokamba Mongo ambaye alifunga bao moja wakati Namungo ikiwaangmiza de Agosto kwa ushindi wa mabao 6: 2

Haya yanajiri baada ya vipimo vya korona kuonesha wachezaji wengine wawili wa timu hiyo wana maabukizi,ukilinganisha na wale watano ambao mapema walikutwa na virusi hivyo.

Daktari wa de Agosto Virgílio Paez, amesema huenda ni hujuma wanafanyiwa.

Namungo watarudiana na De Agosto leo saa 11:00 jioni katika uwanja wa Azam Complex Chamazi.