“Hapa tulipokaa ilikuwa ndio Makao Makuu ya TANROADS Mkoa wa DSM, nikaja nikabomoa, walinishangaa kweli hata ndani ya Serikali walinishangaa, lakini ni ukweli sisi Serikali hatuwezi kuongoza kuvunja Sheria, Sheria ni msumeno, leo pamependeza”
“Jengo hili nilisema kipande hiki cha TANESCO kipo ndani ya Barabara, namkumbuka Mtani wangu Mzee Pinda akiwa Waziri Mkuu akaniambia Mtu anaweza kweli kulivunja jengo la kama lile la TANESCO!?, sasa mwambieni Pinda jengo la TANESCO liko hapa tumelivunja”
“Mwambieni Pinda jengo la TANESCO tumelivunja liko hapa, mtanishangaa mtasema kwamba huyu anamsema aliyekuwa Waziri Mkuu wake, ndio, kwasababu Sheria ni msumeno, haiwezekani ubomoleshe Watu Kimara halafu uache waliovunja Sheria wengine ndani ya Serikali”


You must be logged in to post a comment.