Waziri wa Fedha na Mipango, Dr.Philip Mpango akiwa Hospitalini Dodoma leo

“Shukrani ya kwanza ni kwa Mungu, amenitendea makubwa, kutoka nilikokuwa siku 14 za Madaktari kunihudumia nyumbani mpaka wakanihamishia hapa, acheni Mungu aitwe Mungu, tuendelee kumtukuza, yeye ndio muweza wa yote, amenipa nafasi ya kuendelea kuitumikia Nchi yetu”

“Nimekaa hapa Hospitali ya Benjamini Mkapa Dodoma nikihudumiwa, hapa peke yake leo ni siku ya 14, nilikuja na mtungi kabisa wa Oxygen, sasa mnaniona leo ni siku ya tatu sijawahi kugusa mtungi wa Oxygen”- Waziri Mpango akiwa Hospitalini

“Afya yangu imeimarika vizuri kabisakabisa, Jopo letu la Madaktari wameona nina afya njema, nina uwezo wa kuanza kurudi kuendelea na shughuli za kulitumikia Taifa letu”- Waziri Mpango

“Niwaombe Watanzania Magonjwa yapo mengi, sio mara ya kwanza nabanwa na kifua tangu utoto wangu, Mdogo wangu Nditiye amefariki kwa ajali, vifo ni vingi sana, tutakufa tu popote na kwasababu yoyote ila tuondokane na hii hofu iliyotanda”- Waziri Mpango leo Dodoma

“Wizara ya Afya inatoa maelekezo namna ya kujikinga, kujifukiza, tufanye hivi vitu vinasaidia, lakini tuenzi sana utaalamu wa Ndugu zetu hawa (Madaktari na Manesi wa Kitanzania)”- Waziri Mpango

“Natoa pole kwa waliofariki nikiwa naugua, Wiki mbili nyumbani na Wiki mbili Hospitali, natamani ningeshiriki mazishi ya Maalim Seif, Balozi Kijazi na jana nimempoteza Mwalimu wangu wa pekee Prof. Ndulu, Mdogo wangu Nditiye, natoa pole sana kwa Famili zao”- Mpango

“Kwa nafasi ya pekee namshukuru Rais Magufuli na Familia yake, hakuna siku ambayo Rais hajanipigia simu sio mara moja sio mara mbili, anatuma Wasaidizi wake kufuatilia afya yangu, Familia yake imekuwa inaomba kwa ajili yangu, namshukuru pia Waziri Mkuu na Makamu wa Rais”-

“Nawashukuru Spika, Jaji Mkuu na Viongozi wote, pia nawashukuru Watanzania wote, mara mojamoja nilikuwa napekuwa mitandao ni upendo wa ajabu, nimeonja upendo mkubwa kwa Watanzania”