Taasisi ya Hakimiliki Tanzania (COSOTA) imevitangazia Vituo vyote vya Redio na Televisheni kuacha kucheza kazi za Muziki na Filamu ambazo hazitakuwa zimehakikiwa
Kuanzia Mei Mosi mwaka huu, kazi za sanaa zitakazocheza zitatakiwa kuwa zimehakikiwa na Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA), Bodi ya Filamu Tanzania (TFB) na kusajiliwa COSOTA kwa ajili ya Hakimiliki
Aidha, waandaaji wa Muziki na Filamu wametakiwa kuhakiki kazi zao kwa ajili ya ulinzi. Hatua hizi zimefikiwa ili kulinda kazi za wasanii na wabunifu


You must be logged in to post a comment.