Ligon Mwenye Miaka 83 Aachiwa huru Baada ya Kukaa Gerezani Zaidi ya Miaka 60

Ligon mwenye umri wa miaka 83 aliachiwa kutoka katika gereza la Pennsylvania alhamisi iliyopita baada ya kufungwa maisha mwaka 1953, ilikuwa ni baada ya kupatikana na hatia za mauwaji pamoja na wizi, hatia ambazo binafsi anasema alionewa.

Mwaka huo zilitokea vurugu huko Philadelphia zikihusisha walevi na kupelekea vifo vya watu wawili, Ligon akiwa na umri wa miaka 15 tuu na wenzake wengine wanahukumiwa vifungo vya maisha jela.

Kufungwa inaweza isiwe ajabu, lakini ajabu inakuja pale ambapo mara kwa mara Ligon alikuwa anakataa kutoka jela kwa misamaha ya rais akidai kuwa kwakua hakuhusika kabisa na shutuma hizo basi hawawezi kusema atoke kwa msamaha, msamaha kwa kosa lipi alilofanya?

Mwaka 2012 mahakama mjini humo ilitoa amri ya kupunguziwa vifungo kwa watuhumiwa wote waliohusika na tukio hilo hali iliyopelekea Ligon kumaliza kifungo chake wiki jana baadaa ya kukaa gerezani kwa miaka 68.

Tangu afungwe mwaka 1953 Ligon hajawahi kukata rufaa, hajawahi kuomba adhabu ipunguzwe na mara nyingi alikuwa akigoma kutoka jela kwa misamaha akisema kuwa kwakua hakuuwa wala kuhusika na vurugu sasa msamaha huo ni kwa lipi? hivyo alikuwa tayari kutumika kifungo chote.

Wakati anatoka jela alhamisi iliyopita Ligon alizungumza maneno machache tuu “Hii sio siku ya huzuni kwangu.”