Mwafrika na mwanamke wa kwanza kuongoza Shirika la biashara la dunia

Ngozi Okonjo-Iweala

Dkt . Okonjo -Iweala ameweka historia kuwa mwanamke wa kwanza, na Mwafrika wa kwanza kuongoza WTO.

Muhula wake utaanza tarehe 1 mwezi Machi mwaka 2021.

Mkutano wa baraza kuu la shirika hilo limefikia hatua hiyo baada ya kupitia mchakato wa mchujo uliowahusisha wagombea wanane kutoka duniani kote.

Licha ya kwamba hivi karibuni alipata uraia wa Marekani, alisema kwamba yeye ni raia wa Nigeria na kujivunia kuwa mzalendo – mwafrika aliyekuwa amevaa nguo yenye utambulisho wa Afrika maarufu kama kitenge.

“Wanahitaji kitu tofauti, haiwezekani mambo yakawa yanachukuliwa kama kawaida tu kwa WTO – [wanahitaji] mtu ambaye yuko tayari kufanya mabadiliko na kuongoza.”

Wasifu wake

Dkt . Okonjo -Iweala ameweka historia kuwa mwanamke wa kwanza, na Mwafrika wa kwanza kuongoza WTO
Mwanamama Ngozi Okonjo-Iweala Mwenye Asili ya Afrika Raia Nigeria na Marekani ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Biashara duniani (WTO)

1: Alizaliwa mwaka 1954 nchini Nigeria

2: Alisomea Harvard 1973-76 na kupata PhD yake katika Chuo cha Teknolojia cha Massachusetts (MIT) mwaka 1981

3: Alifanya kazi katika Benki ya Dunia kwa miaka 25 na kupanda ngazi hadi wadhifa ambao ni wa pili kiuongozi kama mkurugenzi (2007-11)

4: Alikuwa waziri wa fedha nchini Nigeria mara mbili – 2003-2006 na 2011-2015 – na mwanamke wa kwanza kushikilia wadhifa huo

5: Alikuwa waziri wa mambo ya nje kwa kipindi kifupi mwaka 2006 na pia mwanamke wa kwanza kushika wadhifa huo

6: Ni mwanachama wa bodi za Twitter, Benki ya Standard Chartered na Shirika la Kimataifa la ushirikiano wa Chanjo Duniani (GAVI)

7: Aliteuliwa na rais Mohammadu Buhari kuwa mgombea wa wadhifa wa WTO Juni 2020.