Bwana Suleiman B Ramadhani Mkazi wa Unguja Zanzibar Amerejesha Pesa Milioni 150 Alizookota Kwa Mmiliki wake aliepatikana nchini Omani

Msamaria mwema Mkazi wa Unguja, Zanzibar Suleiman Bakari Ramadhan Akida amefanikiwa kuzirejesha Tsh. Milioni 150 kwa Mmiliki wake halali baada ya kuziokota zikiwa zimepotezwa

“Tulishirikiana katika swala zima la kusambaza tangazo la uokotwaji wa pesa katika kisiwa cha Unguja”

“Changamoto zilikua nyingi na nimepigiwa simu sana wengi wanasema wamepoteza lakini nimempata Mmiliki wake ambae ni Raia wa Oman baada ya kujibu maswali likiwemo la pesa zilipotea zikiwa kwenye mfuko wa aina gani, tayari nimeshamtumia kwenye account yake na nimelipia 170000 ya ziada ili tu azipate pesa zake zikiwa kamili Milioni 150″