Karim Khan: Achaguliwa kuwa mwendesha mashitaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai-ICC

Wakili wa ngazi ya juu wa Uingereza amechaguliwa kuwa mwenesha mashitaka Mkuu ajaye wa mahakama ya kimataifa ya jinai (ICC).

Karim Khan, mwenye umri wa miaka 50,kwa sasa anaongoza uchunguzi wa Umoja wa Mataifa juu ya uhalifu wa kivita uliotekelezwa na kikundi cha Islamic State nchini Iraq. 

ICC ndio taasisi pekee ya kudumu inayochunguza uhalifu dhidi ya binadamu. 

Bw Khan amepata ushindi wa kura 72 kati ya 123 za nchi wanachama katika awamu ya pili ya uchaguzi, na ataanza muhula wake wa miaka tisa katika mahakama hiyo mjini the Hague mwezi Juni.

Amewashinda wagombea kutoka Ireland, Italia na Uhispania. 

Bw Khan atakuwa ndiye mwendesha mashitaka mkuu wa tatu pekee katika historia ya miaka 18 ya mahakama hiyo, akimrithi Mgambia Fatou Bensouda.

Waziri wa mambo ya kigeni wa Uingereza Dominic Raad amepongeza uchaguzi wake, akisema: ”Uzoef wa Karim katika sheria za kimataifa utakuwa ni muhimu katika kuhakikisha tunawawajibisha wahalifu wakuu na kupata haki kwa wahanga wao”

Tangu mwaka 2018, Bw Khan ameongoza uchunguzi wa Umoja wa Mataifa uliolenga kuwatambua na kuwafikisha mbele ya sheria waliohusika na maasi ya Islamic state nchini Iraq. 

Katika kazi yake ya sheria ya miaka 27, aliwahi kufanya kazi kama mwendesha mashitaka katika Mahakama ya Kimataifa kwa ajili ya uhalifu uliofanyika wakati wa vita katika Yugopslavia ya zamani na wakati wa mauji ya kimari ya Rwanda.

Na pia amewahi kuwamtetezi wa watu kama vile Naibu rais wa Kenya William Ruto katika mahakama ya ICC – ambayo ilitupa nje mashitaka ya mauaji, kusafirisha na mateso kufuatia uchaguzi wa mwaka 2007 – na mwanae akiongozi wa Libya Muammar Gaddafi, Saifd Al Islam.

Miongoni mwa majuku yake ya kwanza kama mwendesha mashitaka mkuu wa ICC itakuwa ni kuamua jinsi ya kushughulikia uchunguzi wenye utata kuhusiana na uhalifu wa kivita, na huenda katika eneo lililovamiwa la Wapalestina.

Mwaka jana Marekani-ambayo pamoja na Uchina na Urusi haziitambui mahakama hiyo, ilimuwekea vikwazo mwendeshamashitaka wa sasa Bi Bensouda wakati alipojaribu kuchunguza vitendo vya Marekani nchini Afghanstan.

Na Israeli- ambayo pia sio wanachama wa ICC-iliishutuma mahakama hiyo kwa kuingilia ”haki za kidemokrasia za nchi za kujilinda binafsi ” wakati ilipotoa uamuzi kuwa ina mamlaka ya kisheria ya kufuatilia uhalifu wa kivita na maasi yaliyofanyika ndani ya mipaka ya Wapalestina.