Ni baada ya Mamlaka kudai Wachezaji watatu na Kiongozi mmoja wana maambukizi ya Virusi vya Corona
Namungo ipo Angola kuchuana na Clube Desportivo 1º de Agosto katika mechi ya kombe la shirikisho.
Namungo FC imezuiliwa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Luanda nchini Angola baada ya mamlaka kudai wachezaji watatu na kiongozi mmoja wana virusi vya Corona.
Imeripotiwa kuwa, Mamlaka za Angola zimeutaka msafara mzima kurejea Tanzania au kukaa karantini