Jurgen Klopp kujaribu kumsajili mshambuliaji wa Udinese Rodrigo de Paul ili kuipa makali zaidi safu yake ya ushambuliaji.

Winga wa klabu ya Borussia Dortmund na timu ya taifa ya England Jadon Sancho, 20, amejihakikishia kuwa tacheza klabu nyengine msimu ujao lakini kuna matumaini finyu juu ya miamba ya Dortmund kumuuza kwa pauni milioni 100 ambazo walikuwa wakitaka Manchester United wazitoe miezi sita iliyopita. (Eurosport)

Klabu ya Liverpool wanajiandaa na kuondoka kwa kiungo wao mkabaji, Mholanzi Georginio Wijnaldum, 30, na wanataka kumsajili kiungo wa Borussia Monchengladbach Florian Neuhaus, 23, kama mrithi wake. (Kicker) 

Kocha wa wa Liverpool Jurgen Klopp pia anatarajiwa kujaribu kumsajili mshambuliaji wa Udinese na raia wa Argentina Rodrigo de Paul, kwa dau la pauni milioni 30. (Sun)

Jurgen Klopp

Arsenal wanaamini wanaweza kumsahwishi mshambuliaji kinda wao Folarin Balogun, 19, kusaini mkataba mpya. Mkataba wa mshambuliaji huyo wa England unafikia ukomo mwishoni mwa msinu na tayari kuna klabu kadhaa barani Ulaya zinazomnyatia. (London Evening Standard)

Klabu za Ujerumani Bayer Leverkusen na Stuttgart pamoja na Rennes ya Ufaransa ni baadhi ya timu zinazomuwania Balogun. (Mirror)

Mlinda mlango wa Aston Villa Emiliano Martinez amemlinganisha kiungo wa Villa Jack Grealish, 25, na nyota wa Barcelona Lionel Messi. (Talksport)

Klabu ya Bournemouth ambayo haina kocha kwa sasa imeshauriwa na mchezaji nguli wa zamani wa Arsenal Martin Keown kumsajili kiungo nguli wazamani wa Arsenal Patrick Vieira, 44, awe kocha wao mpya. (Talksport)

Klabu za New York Red Bulls na DC United zote za Marekani zinapima mizani kabla ya kujitosa katika mbio za kumsajili beki wa West Bromwich Albion Kieran Gibbs, 31, ambaye tayari anawaniwa na Inter Miami ya Marekani pia. (ESPN)

Mshambuliaji wa Uhispania Diego Costa, 32, ambaye aliondoka Atletico Madrid mwezi Disemba, yupo katika mazungumzo ya kujiunga na klabu ya Palmeiras ya nchini Brazil ambayo alikuwa akiishabikia utotoni. (Sky Sports)

Beki Mfaransa Lucas Digne, 27, amekubali kuingia mkataba mpya na klabu yake ya Everton. (Sky Sports)