“Billnass nilikutana naye mara ya kwanza kwenye basi la ‘tour’, nilikuwa nasikia ananipenda sana sasa siku hiyo baada ya kukutana akanijaza sana kuwa ananikubali najua kuimba” – Nandy
“Siku hiyo baada ya show tuko chumbani na Maua Sama, Billnass akaja akamtonya Maua akaondoka akatuacha 2, tukaongea mambo mengi. Nikamuona msichana wake wa Kiarabu akajitetea sana, nikamuambia malizana naye huyo kwanza”- Nandy
“Huwa napenda sana kushika simu ya mpenzi wangu, lakini sijawahi kukuta chochote ninachokitafuta. Nililazimika kumuuliza Ex wake kuwa kwenye mahusiano yao tatizo lake lilikuwa ni nini, akaniambia vitu vingine kabisa” – Nandy