Mbunge wa Viti Maalum Najma Giga amesema talaka za ovyo zimezidi Nchini Tanzania na kama hili swala halitofanyiwa kazi kwa mkazo itakua janga kubwa zaidi siku zijazo.

“Nchi yetu bado ina changamoto kwenye mporomoko wa maadili kwenye jamii lakini nawashukuru walioiandaa ILANI ya CCM kwani wamefafanua tutaondokana vipi na mporomoko wa maadili ukurasa wa 44 na 45”

“Mimi nitakua sambamba na Mawaziri kwenye miaka hii mitano kuhakikisha vile vifungu vyote kwenye ILANI tunavishughulikia ipasavyo mporomoko wa maadili ikiwemo mimba za utotoni, pia swala la talaka za ovyo Nchi yetu imezidi”

“Jamani talaka za ovyo Nchi yetu imezidi tunashindwa kudumisha ndoa zetu na badala yake tunatelekezwa kwa familia zetu na Watoto wetu ambao mwisho wa siku ndio wanakwenda kupata mimba za utotoni”