Rwanda yasema Taarifa ya Uingereza haina uchunguzi wa Kisayansi

Nchi ya Rwanda imetoa taarifa ikiitaka Uingereza kutoa sababu zenye mashiko zilizopelekea kuwapiga marufuku wasafiri kutoka Rwanda wasiingie Uingereza.

Hatua hii ya Rwanda inakuja baada ya Uingereza kuiongeza Rwanda, Burundi na Umoja wa Falme za Kiarabu kwenye orodha ya wasioruhusiwa kuingia Uingereza kisa kudhibiti Corona.

Rwanda imesema imechukua tahadhari zote dhidi ya Corona kwa Kupima, kufuatilia waliokutana na wenye maambukizi, kuwadhibiti wenye maambukizi, kuwapima Covid 19 Wasafiri wote wanaoondoka na wanaopitia Nchini humo nk

“Taarifa ya Uingereza haina uchunguzi wa Kisayansi, pia tuwakumbushe Uingereza kuwa wakati Mataifa mengine yalipowapiga marufuku Wasafiri wa Uingereza kutoingia Nchini mwao kutokana na kirusi kipya cha Corona kilichogundulika Uingereza mwaka jana, sisi hatukuwazuia kuja kwetu”-taarifa kutoka Rwanda