Wakati Rais Dkt John Pombe Magufuli anaingia madarakani na muda mfupi baadaye 2017 kutangaza azma ya Serikali yake kutekeleza mradi mkubwa wa kuyatoa maji kutoka Ziwa Victoria mpaka kwenye mikoa ya Shinyanga na Tabora katika miji ya Kahama, Isaka, Tabora Mjini, Nzega na Igunga, hakuna mtu aliyeamini wala kukubaliana na hilo na wengi walidhani na kusema suala hilo ni ndoto tu na haliwezi kufanikiwa kamwe!

Wengi walidhani ni ahadi tu na stori za abunuasi kwa Tanzania kutekeleza mradi huo mkubwa wa kuyatoa maji takribani zaidi ya Km 281 kutoka Ziwa Victoria kwa Mabillion ya fedha kufika Shinyanga na Tabora. Wengi walibeza sana na kukataa kata kata suala hilo huku wakidai jambo hilo ni kuhadaa tu wananchi.
Sasa hayawi hayawi sasa yamekuwa na waliosema hayawi leo yamekuwa na yameonekana. Waliosema ni ndoto tu na stori za abunuasi leo wamejionea wenyewe ambapo mradi huo mkubwa kabisa kuliko mradi wowote wa maji nchi nzima ya Tanzania wenye thamani ya ya billion 617 umezinduliwa rasmi na Rais Dkt John Pombe Magufuli ambao utapeleka maji kwenye miji ya Tabora mjini, Nzega na Igunga na ule mwingine wa kupeleka maji kwenye miji ya Kagongwa na Isaka.
Miradi hiyo yote miwili ya kutoa maji Ziwa Victoria ambayo imegharimu Billion 640.1 itahudumia wananchi zaidi milioni 1.3 wa maeneo hayo na kumaliza kabisa tatizo sugu na la muda mrefu la maji katika eneo hilo ambapo mradi wa Billioni 617 unazalisha lita milioni 54 za maji kwa siku wakati mahitaji ya maji kwa miji ya Tabora, Nzega na Igunga na vijiji vingine 102 yakiwa ni lita milioni 37 tu kwa siku hivyo kuwa na ziada ya lita milioni 17 kapuni huku ule wa Kagongwa na Isaka ukizalisha lita 9,832,600 wakati mahitaji ya wananchi yakiwa lita 4,609,000 na hivyo kuwa na ziada ya maji lita 5,223,600.
Nani alisema maji ya Ziwa Victoria hayafiki Shinyanga na Tabora?
You must be logged in to post a comment.