Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kupitia kituo chake cha Televisheni cha TBC1 na cha Redio ya TBC Taifa, imepata Tuzo kutokana na matumizi fasaha ya lugha ya Kiswahili na ulindaji wa madili ya Mtanzania
TBC pia imepewa hati ya shukrani kwa kutambua na kuthamini mchango wake wa hali na mali katika kufanikisha maadhimisho ya Siku ya Kiswahili (MASIKI) huko Dodoma.