Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) limesitisha Mafunzo

Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) limesitisha mafunzo ya kujitolea ya mwaka 2020/2021 kwa vijana takribani 12,000 yaliyokuwa yaanze hivi karibuni katika kambi mbalimbali nchini kutokana na sababu za ndani ya jeshi hilo mpaka hapo litakapo tangaza tena.

Tamko hilo limetolewa kwenye makao makuu ya jeshi hilo Chamwino mkoani Dodoma na Kaimu Mkuu wa Utawala wa JKT, Kanali Hassan Mabena.