PICHA YA LEO : Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa kwenye picha ya pamoja na wanafunzi

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa kwenye picha ya pamoja na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Bukoba mara baada ya hafla ya utiaji saini Mkataba wa Ubia wa Uchimbaji madini aina ya Nickel kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Kampuni ya uchimbaji madini ya LZ Nickel ya nchini Uingereza.

Hafla hiyo ilifanyika katika shule ya Sekondari Bukoba mkoani Kagera. Rais Magufuli aliambatana na Mawaziri, Makatibu Wakuu na viongozi wengine wa mkoa wa Kagera.