Mapigano yasababisha vifo vya watu zaidi ya 45

Ghasia kati ya makundi ya kikabila katika jimbo la Magharibi mwa Darfur zimesababisha mauaji ya watu 50, kulingana na chombo cha habari cha Sudan kikinukuu muungano wa madaktari.

Mapigano katika mji mkuu wa jimbo hilo , Elgeneina , yalianza siku ya Jumamosi baada ya mzozo ambapo mtu mmoja alidungwa kisu hadi kufa.

Masharti ya kutotoka nje yamewekwa na waziri mkuu Abdalla Hamdok ametuma ujumbe kuchunguza.

Mzozo wa Darfur ulioanza mwaka 2003 ulipelekea mamlioni ya watu kutoroka eneo hilo na licha ya makubaliano ya amani kuna hali ya taharuki.

Ghasia za Jumamosi zinajiri chini ya wiki , baada ya walinda amani kutoka Umoja wa Mataifa na vikosi vya Umoja wa Afrika kukabidhi serikali ya Khartoum jukumu la Usalama Ikiwa Vikosi hivyo vimekuwa Sudani kwa takriban miaka 13.

Ghasia kama hizo katika eneo la El Geneina mwaka uliopita , ambazo zilisababisha vita kati ya wafugaji wa Kiarabu na wale wasio Waarabu zilisababisha mauaji ya zaidi ya watu 100.