Mkuu wa Wilaya ya Kahama Anamringi Macha amesema Serikali imepiga marufuku uuzaji, usafirishaji na ulaji wa nyama ya nguruwe (Kitimoto) kwa muda usiojulikana Wilayani humo baada ya kujitokeza kwa ugonjwa wa homa ya nguruwe ambao umesababisha vifo vya nguruwe zaidi ya 800.

“Tumelazimika kuchukua hatua hiii ili kudhibiti kuenea kwa maambukizi ya ugonjwa huo ambao unaua nguruwe kwa kasi, watakaobainika kukiuka agizo hili watachukuliwa hatua kali za kisheria”-
“Kwa sasa Kahama biashara ya nguruwe imepigwa marufuku, lengo letu ni kudhibiti ugonjwa huu, Wataalamu wetu wanaendelea kufanya utafiti ili kuhakikisha wanaudhibiti mapema ili kuzuia madhara yasijitokeze zaidi”
“Walaji wa nyama ya nguruwe (Kitimoto) acheni kula nyama hiyo hadi mtakapotangaziwa na Serikali, kuleni nyama nyingine kama za ng’ombe , mbuzi, kondoo na kuku ambao ugonjwa huu haujawaathiri”
You must be logged in to post a comment.