Makocha wengi wameomba kazi ya kuiongoza Simba, ambayo ni timu ya juu lakini nimeshangazwa kuona kwamba hakuna kocha mzawa aliyeomba kazi
Kazi hii pia inaweza kufanywa na makocha wetu wa hapa lakini ni bahati mbaya kwamba hakuna hata mmoja aliyeonyesha nia, nataka wajitokeze pia kuomba.
Makocha wetu wa hapa wanapaswa pia kujiamini na kujaribu kufanya kazi na timu ambazo zina shinikizo, wanapaswa kujipima na timu ambazo zina mashabiki wengi.
Amesema CEO wa Simba SC Barbara Gonzalez.