
Klabu ya Simba inafanya mazungumzo na aliyewahi kuwa Mkufunzi Mkuu wa Timu ya Taifa ya Uganda Sebastien Desabre raia wa Ufaransa mwenye umri wa miaka (44) kuchukua jukumu la ukufunzi katika klabu hiyo baada ya Kuondoka kwa Sven Vanderbroeck
Kulingana na taarifa kutoka kwa vyombo vya habari kutoka Tanzania, Simba SC inafanya mazungumzo na Kocha Mkuu wa Uganda Cranes Sebastien Desabre kuchukua jukumu la ukocha katika kilabu hicho.
Awali Simba SC iliwasilisha ofa ya mshahara ya dola 13,000 za Kimarekani kwa mwezi kwa kocha huyo wa zamani wa Pyramids FC lakini alikataa kudai Dola za Kimarekani 22,000 kwa mwezi.
You must be logged in to post a comment.