PICHA YA LEO: 18 Januari 2021

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Askofu Msaidizi wa Kanisa Katoliki Jimbo la Bukoba Methodius Kilaini, Askofu wa KKKT Dayosisi ya Kaskazini Magharibi Dkt. Abednego Keshomshahara, Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Bukoba Desiderius Rwoma, Shehe wa Bukoba Mubarak Juma pamoja na Padre Revocatus Mwehuzi muda mfupi mara baada ya kupata chakula cha Mchana katika Ikulu ndogo ya Bukoba mkoani Kagera.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa amewashika mikono Balozi wa Uingereza hapa nchini David Concar pamoja na Balozi wa China hapa nchini Wang Ke muda mfupi baada ya kupata chakula cha Mchana katika Ikulu ndogo ya Bukoba mkoani Kagera.

Baaada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli kutoa maagizo kwa Viongozi wa Serkali kutimiza wajibu wao katika kuwatumikia wananchi.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Aboubakar Kunenge, mapema leo jioni ,amewasili katika shule ya Msingi King’ongo,na kujiona uhalisia wa shule hiyo,pamoja na kuanza kuifanyia ukarabati,kama agizo la Rais Magufuli lilivyowataka Viongozi hao.