Kiongozi wa Chama Cha ACT Wazalendo Ndugu Zitto Kabwe amekutana na kufanya mazungumzo na Wabunge wa Bunge la Jamhuri wa Muungano wa Tanzania kupitia ACT Wazalendo, leo tarehe 14/01/2021, katika Ofisi ya Chama Cha ACT Wazalendo iliyopo Magomeni, Jijini Dar es Salaam.
Kwenye kikao hicho Kiongozi wa Chama aliwataka Wabunge hao kuhakikisha wanafanya kazi zao za kuwawakilisha wananchi kwa maslahi ya Wananchi wa pande zote mbili za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Aidha yeye Kama Kiongozi na Msemaji Mkuu wa Sera za Chama atakuwa pamoja nao katika utekelezaji wa majukumu yao na alitaka Idara ya Bunge, Baraza la Wawakilishi kuhakikisha wanafanya kila linalowezekana ili Wabunge hao wa Wananchi wanatimiza wajibu wao kwa Chama, majimbo yao na Nchi kwa ujumla.
Kikao hicho kilichohudhuriwa pia na Makamo Mwenyekiti Bara Dorothy Semu, Katibu Mkuu Ado Shaibu, Naibu Katibu Mkuu Joran Bashange na Katibu wa Idara ya Chama ya Bunge, Baraza la Wawakilishi na Serikali za Mitaa Hamad Yusuph, kimefanyika huku Wabunge hao wakijiandaa kushiriki katika vikao vya Kamati za Kudumu za Bunge zinazotarajiwa kukutana hivi karibuni Mjini Dodoma.
Hamad Yusuph, Katibu wa Kamati ya Bunge, Baraza la Wawakilishi na Serikali za Mitaa, ACT Wazalendo..

You must be logged in to post a comment.