NYUMBA ZA MAGOMENI KUKABIDHIWA MWISHO WA MWEZI HUU

Wakala wa Majengo Nchini (TBA) imeahidi kukamilisha ujenzi wa nyumba za kota za Magomeni mwisho mwa mwezi huu tayari kwa kukabidhiwa kaya 644 ambazo ni zaidi ya wakazi 3000 watakaoishi hapo.

Meneja mradi huo, Benard Mayemba kutoka TBA ameeleza hayo kwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, alipotembelea mradi huo kwa lengo la kujionea maendeleo yake na kuwataka kumaliza kwa wakati na kutoa elimu kabla wahusika hawajahamia kutokana na ukweli kwamba miudombinu mingi iliyopo kwenye nyumba hizo ni ya kisasa tofauti ya awali.