LAO NI FAINALI YA KISASI IKIWA IMEPITA MIAKA KUMI

Yanga atalipa kisasi baada ya miaka 10 Au Mnyama ataendeleza ubabe?

Ni miaka 10 imepita tangu watani wajadi, Simba na Yanga wakutane kwenye fainali ya kombe la Mapinduzi.

January 2011 Simba alimfunga Yanga kwenye fainali ya kombe la Mapinduzi kwa matokeo ya 2-0. Magoli ya Mussa Mgosi dakika ya 33 na Shija Mkinna dakika ya 71 yalimsaidia mnyama kuondoka na kombe la Mapinduzi kwenye uwanja wa Amaan Zanzibar.

Miaka 10 baadae, January 2021 kwenye dimba lile lile, Simba na Yanga wanakutana kwenye fainali ya kombe la Mapinduzi.