Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Damas Ndumbaro ameitangaza Chato kuwa Kitovu Kikuu cha Uhifadhi na Utalii Kanda ya Ziwa kwakuwa ina vivutio vingi vya utalii na kwa kuwa Chato ni eneo tulivu, amesema hayo wakati akikagua shamba la miti la Biharamulo.

“Chato kuna Utalii wa aina nyingi unaweza kufanya utalii wa misitu, kuna Ziwa unaweza kufanya utalii wa maji, kuna hifadhi ya Burigi Chato unaweza kufanya Utalii wa kupiga picha, kutazama Wanyama na uwindaji”

“Chato wana Uwanja wa Ndege na Watalii wanahitaji usafiri wa uhakika, unaweza kuingia Chato kwa usafiri wa Ndege na kupitia majini lakini pia ni sehemu tulivu na Watalii wanapenda utulivu”Alisema Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Damas Ndumbaro
Nini Maoni yako?
You must be logged in to post a comment.