Mchezo ambao watu wanauhusisha moja kwa moja na ulimwengu wa kishetani.
Kama ni mtumiaji mzuri wa mitandao ya kijamii kwasasa utakuwa si mgeni kwenye mchezo mpya unaotamba kwasasa maarufu kama Charlie Charlie challenge

Inaaminika kwamba jina hilo ni la mizimu kutoka nchi ya Mexico ijapokuwa watu wa Mexico wanakanusha kutokuwa na jina la aina hiyo.
Mchezo huo umekuwa ni wa kuogopesha kiasi cha kupelekea baadhi ya nchi kupigwa marufuku.
Mchezo huo umekuwa ukichezwa zaidi mashuleni na vyuoni, ambapo inaripotiwa wanafunzi wengi wanashuhudia mambo yasiyo ya kawaida yakitokea pindi wanapocheza mchezo huo kama watu kudondoka ghafla, kutapika na hata vifo.
Viongozi mbalimbai wa kidini akiwepo aliyekuwa kiongozi wa dhehebu la kievangelisti Marekani Bill Graham walijitoa kupaza sauti kuwasihi wazazi kuto waruhusu watoto wao kushiriki katika mchezo huo kwani unahusisha ulimwengu mwingine wa kiroho na wafu na unaweza kumdhuru mtu mmoja kama si wote.
You must be logged in to post a comment.