Cristiano Ronaldo na Josef Bican ni wachezaji wanaoshikilia rekodi ya ufungaji wa magoli mengi katika historia ya kandanda Duniani

Cristiano Ronaldo kwa sasa ndio mfungaji wa magoli mengi katika historia ya soka duniani kulingana na ripoti baada ya kufunga bao lake la 759 akiichezea Juventus dhidi ya Sassuolo ambapo timu yake iliibuka na ushindi wa magoli 3- 1. Lakini je ni kweli?
Ronaldo amefunga magoli matano akiichezea Sporting Lisbon , 118 akiichezea Man United, 450 akiichezea Real Madrid, 84 akiichezea Juventus na 102 akiicheza timu yake ya taifa ya Portugal – hivyobasi hakuna shaka kuhusu magoli aliyofunga.

Lakini tatizo linaonekana kutoka katika wapinzani wake wa siku za nyuma.
Data kutoka Rec.Sport.Soccer Statistics Foundation (RSSSF) zinasema kwamba Josef Bican ndio mfungaji wa magoli mengi katika historia ya kandanda , mbali na wachezaji ambao hawajashiriki soka ya kiwango cha juu akiwa na magoli 805 kutoka kwa mechi 305 pekee , huku naye Romario akiwa na magoli 772 naye Pele akiwa na magoli.
Bican, aliyefariki mwaka 2001, alichezea klabu tano ikiwemo Rapid Viena na Slavia Prague pamoja na Austria na Czechoslovakia – katika kazi alioanza 1931 hadi 1955.
Lakini miongoni mwa magoli 805 aliofunga kulikuwa na magoli 27 yaliofungwa katika timu ndogondogo pamoja na magoli ambayo hayakutokana rasmi mechi za kimataifa.
Ondoa magoli hayo na itabainika kwamba Bican alimaliza kipindi chake cha uchezaji soka na magoli 759 . Pengine huenda RSSSF inasema kwamba baadhi ya data huenda zinakosekana kuhusu ligi ya daraja la pili ya taifa la Czech 1952.
Hivyobasi tunauliza je ni magoli mangapi aliofunga Pele na Romario? Kuna mzozo Kuhusu jumla ya magoli huku wachezaji wote hao kutoka Brazil wakidai kufunga magoli 1,000 ..

Mshambuliaji nyota wa klabu ya Barcelona Lionel Messi hivi majuzi alivunja rekodi ya Pele ya 643 akiichezea klabu moja …lakini Santos inasema kwamba magoli ya Pele katika mechi za kirafiki yanajumlisha idadi hiyo kufikia magoli 1,091 akiichezea klabu .

Katika akunti yake ya Instagram Pele anasema kwamba ndiye mfungaji bora wa magoli katika historia ya kandanda akiwa na magoli (1,283)”.
Lakini ukiondoa magoli ya mechi za kirafiki na yale yasio rasmi ikiwemo wakati mmoja 1959 alipoichezea timu ya jeshi, magoli yake 757 akiichezea Santos, Brazil na New York Cosmos huenda ndio yanayosababisha kizungumkuti hicho.
Romario alisherehekea kufunga goli lake la 1,000 mwaka 2007 – lakini hilo lilishirikisha mechi za vijana pamoja na zile za kirafiki.
Raia huyo wa Brazil ana sifa za kufunga magoli 745 katika kipindi cha mchezo kilichoshirikisha Marekani ya Latini, Ulaya, bara Asia na Australia – ijapokuwa jumla ya magoli hayo inaonekana kubadilika kutoka ripoti moja hadi nyingine.
Hivyobasi ili kujibu swali hilo , pengine Ronaldo ndiye anayeshikilia rekodi ya watu wawili ya ufungaji wa magoli mengi zaidi. Lakini hakuna hakika.
Tunajua kwamba Messi ana magoli 40 nyuma ya Ronaldo baada ya kufunga magoli 719 akiichezea Barcelona na Argentina katika enzi ambapo takwimu hurekodiwa rasmi..
Wiki hii, Ronaldo ana fursa kuvunja rekodi hiyo siku ya Jumatano ambapo Juventus itakuwa inacheza dhidi ya Genoa.
Cristiano Ronaldo kwa sasa ndiye mfungaji wa magoli mengi katika historia ya soka duniani kulingana na ripoti, baada ya kufunga bao lake la 759 akiichezea Juvetus dhidi ya Sassuolo ambapo timu yake iliibuka na ushindi wa magoli 3- 1.
You must be logged in to post a comment.