Polisi nchini Kenya wanaendelea na msako dhidi ya wezi waliiba na kupika Ugali na Kula

Polisi mjini Nyamira nchini Kenya inawasaka wahalifu nane wenye uthubutu wa kupitiliza ambao waliingia kwenye nyumba moja,kwa lengo la kuiba,lakini baada ya kutekeleza tukio hilo, wezi hao walipitiliza hadi jikoni ambapo walichukua nyama ulivyokuwa imehifadhiwa kwenye jokofu pamoja na unga wa ugali,na kujipikia ugali kwa nyama .
Baada ya kushiba wezi hao,wakaishuruku familia hiyo kwa ushirikiano na kutokomea na mali waliyoiba katika Nyumba hiyo.
Kulingana na ripoti ya polisi, kisa hicho kilitokea jumanne usiku katika kijijini Bomondo, ambapo wezi hao walimvamia Stephen Gichana alipokuwa akisubiri kuingia katika lango la nyumba yake ,lakini kabla hajafanya hivyo, genge la watu naane waliovalia jaketi lilimvamia na kumpiga utosini kwa kifaa butu, na kumuamuru mtoto wa Gichana afungue geti hilo.
Wahalifu hao walipoingia ndani ya nyumba waliwafunga kwa kamba Gichana, mkewe na Mtoto wao.
You must be logged in to post a comment.