Ziara ya Rais wa Msumbiji Nchini Tanzania

“Rais Nyusi alinipigia simu anataka kuja Chato alisikia nipo hapa, nikamwambia njoo, nashukuru Nyusi kwa kuamua kuja Chato, unayajua maisha ya Tanzania na ni Rafiki wa muda mrefu wa Tanzania, sisi na Msumbiji ni Ndugu na tuna makubaliano ya kushirikiana”-JPM

“Biashara kati ya Tanzania na Msumbiji imeongezeka, hadi kufikia mwaka 2020 ilifikia Tsh. Bilioni 93.6, kuna makampuni ya Msumbiji yanafanya kazi hapa na baadhi ya makampuni ya Tanzania yanafanya kazi kule” -JPM

“Nawapongeza Wakandarasi, Wizara ya Fedha na pia Wizara ya Afya kwa kutaka Hospitali hii ya Rufaa ya Kanda ya Chato iwekwe jiwe la msingi na Nyusi, ila nitawabana kweli ili ikamilike mara moja, ni Hospitali kubwa itahudumia zaidi ya Watu Mil 18 Tanzania na Nchi za jirani” – JPM

“Nawapongeza Wakandarasi, Wizara ya Fedha na pia Wizara ya Afya kwa kutaka Hospitali hii ya Rufaa ya Kanda ya Chato iwekwe jiwe la msingi na Nyusi, ila nitawabana kweli ili ikamilike mara moja, ni Hospitali kubwa itahudumia zaidi ya Watu Mil 18 Tanzania na Nchi za jirani” – JPM

“Nilipiga simu juzi kumuuliza Rais Magufuli uko wapi, na mara nyingi tunaongea asubuhi mapema, akasema yupo Chato, nikamuuliza Chato ni wapi? akasema CHATO nyumbani, nikamwambia nakuja kuona kwenu, shule uliyosoma, akasema njoo, nikamwambia sili sembe nakula ugali wa kusaga akasema nitakusagia”-Filipe Nyusi,Rais wa Msumbiji

“Nakupongeza Rais Magufuli kwa kujenga Hospitali hii ya Rufaa ya Kanda ya Chato, Hospitali hii haina Chama itatumiwa na wote, nashukuru kwa kunipa heshima ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Hospitali hii, nitakuwa napiga simu kila Jumamosi kuulizia ujenzi umefikia wapi”-Filipe Nyusi,Rais wa Msumbiji

“Wakati najiandaa na Kampeni za Urais nilikuja Tanzania, Mama Maria Nyerere alinipokea akanipikia mbuzi nyumbani kwake, akaniambia ukiwa Rais, ukishindwa vingi angalau ujenge kiwanda kimoja cha dawa, kwahiyo nakupongeza Rais Magufuli, kwa kushughulika na afya za Wananchi, afya muhimu”-Filipe Nyusi,Rais wa Msumbiji

“Tunaweza kusema kila kitu ila bila maisha yote tunayosema hayatoeleweka, Magifuli ni Rais mzuri, anashughulika na maisha ya Watanzania kutafuta nyumba nzuri, chakula, maji, afya na akiomba afya anataka ile afya ya Quality, hii ni zawadi Kwetu kuweka jiwe la msingi la Hospitali ya Rufaa Chato”-Filipe Nyusi,Rais wa Msumbiji