Nusu Fainali ya kombe la mapinduzi kuchezwa leo huko Zanzibar
Timu za Ligi kuu Tanzania Bara zimefuzu Mchezo wa Mapema hii leo Unawakutanisha Matajiri wa Chamazi na wapiga mbizi Jagwani .
1. Nusu Fainali Mapinduzi Cup
Young Africans Sc VS Azam Fc
Mchezo wa pili Unawakutanisha Vijana wa Ruhagwa mbele ya Mnyama mkali kabisa na hatari zaidi Wekundu wa Msimbazi
2.Nusu Fainali Mapinduzi Cup
SIMBA SC vs NAMUNGO FC
Historia ya Mashindano haya hadi sasa Mapinduzi Cup 2021
- Yanga ndiyo timu pekee ambayo haijaruhusu bao lolote hadi sasa.
- Yanga ndiyo timu pekee ambayo haijatumia wachezaji waliokuja kufanya majaribio au waliosajiliwa dirisha dogo.
- Simba ndiyo timu pekee iliyoshinda mechi zote na kuingia na pointi zote sita kutoka hatua ya makundi.
- Simba ndiyo timu iliyofunga magoli mengi zaidi ya mawili (magoli matano), ikifuatiwa na Azam pamoja na Namungo zenye magoli mawili kila timu.
- Simba ndiyo timu pekee inayoingia hatua hii bila ya kuwa na kocha mkuu.
- Miraji Athuman wa Simba ndiye kinara wa mabao hadi sasa akiwa na magoli matatu.
- Namungo ndiyo timu pekee ambayo inashiriki michuano hii kwa mara ya kwanza.
- Azam ndiyo timu pekee iliyochukua kombe hili mara nyingi zaidi kuliko timu yoyote.
- Kama Azam akipoteza Mchezo wake Yanga akaibuka Mshindi basi Kutakuwa na Uwezekano mkubwa wa Simba na Kukutana fainali 13/01/2021