NANI BIGWA WA MAPINDUZI CUP

Fainali ya kombe la mapinduzi imewakutanisha vigogo wa soka la Tanzania watani Wajadi Simba na Yanga yaani Vijana wa Kiafrika na Mnyama hatari zaidi duniani

MAPINDUZI CUP FINAL

YANGA SC vs SIMBA SC

Yanga imefuzu kwenye nusu fainali ilipocheza na Azam FC na kuibuka na ushindi wa penalti 5-4 baada ya matokeo ya dakika 90 zikimaliza kwa sare ya bao 1-1.

Nyota ya Miraji Athuman na Meddie Kagere wa Simba wemeendelea kung’ara kwenye mashindano ya Kombe la Mapinduzi ambapo wameisaidia timu kuvuka hatua ya fainali ambapo sasa watacheza na Yanga Jumatano Januari, 13 kwenye Uwanja wa Amaan kisiwani Zanzibar .

Mchezo huo utakachezwa kiwanja cha Amani unakuwa na mvuto zaidi kwa sababu timu hizo ni Mahasimu wa Muda mrefu Na ni mchezo wa kwanza Mwaka huu kuwa kutanisha Watani Wajadi