NDEGE YA INDONESIA ILIANGUKA BAHARINI

Ndege ya abiria Sriwijaya Air, iliyokuwa na Watu 62 imeangukia baharini muda mfupi baada ya kuruka kutoka uwanja wa Ndege wa Jakarta nchini Indonesia na zoezi la kutafuta miili ya Binadamu na mabaki ya Ndege linaendelea.

Waziri wa usafirishaji wa Indonesia Budi Karya Sumadi amesema ndege hiyo aina ya Boeing chapa 737-500 ilipoteza mawasiliano dakika nne baada ya kupaa na miongoni mwa abiria waliokuwamo ni watoto saba.

Ndege hiyo ilikuwa ikielekea Pontianak kwenye kisiwa cha Borneo., Wavuvi wamebaini vipande vya chuma ambavyo vinaaminika kuwa sehemu ya Ndege hiyo.

Indonesia iliyo na wakaazi zaidi ya milioni 260, imekuwa ikikabiliwa na ajali za usafiri kutokana na ubovu wa miundombinu na utekelezwaji hafifu wa sheria za usalama, Mwaka 2018, Boieng chapa Max 8 ya Lion air ilianguka na kuwaua watu 189 waliokuwamo ndani.