
Rekodi ya juu zaidi kwa Simba katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika ni hatua ya nusu fainali, ambayo walicheza mwaka 1974 ambapo ilibaki kidogo watinge fainali lakini walifungwa kwa mikwaju ya penati 3-0 na Ghazl Al-Mahalla ya Misri.

Msimu wa 2018/19 ilikutana na Al-Ahly na Vita Club ya DRC ambao wapo kwenye kundi A tena msimu huu. Timu ya nne katika kundi hilo ni miamba ya Sudani El Merreikh.

Walipokutana mara ya mwisho, Simba na Al Ahly ndiyo waliovuka kwenda hatua ya robo fainali.
Simba wamekuwa na rekodi nzuri nyumbani, katika msimu wa 2018/19 walifungwa goli 5 na Ahly na Vita walipokuwa ugenini, lakini Simba ilizifunga timu zote hizo jijini Dar Es Salaam.
Katika hali yoyote ile, kundi hilo ni gumu na klabu zote zitatakiwa kupambana kwa hali na mali kufuzu.
Simba inasifika kwa kuwa wakali nyumbani, na toka msimu wa 2018/2019 haijawahi kufungwa nyumbani katika michuano hiyo.
Alama zote 9 walizopata msimu wa 2018/19 na kufuzu kwenda robo fainali walizipata katika uga wa Mkapa.

Kutokana na rekodi hiyo ya Simba, ni dhahiri kuwa timu zote zitajikaza na kupambana zaidi watakapocheza jijini Dar Es Salaam.
Endapo Simba itafuzu katika hatua ya makundi, itasonga mpaka hatua ya robo fainali.

Hiyo ni hatua kubwa lakini si hatua kubwa zaidi kuwahi kufikiwa na Simba.
Simba imefika mara nne hatua ya robo fainali, mara ya mwisho ikiwa ni msimu wa 2018/19 ambapo walitolewa na miamba ya DRC TP Mazembe baada ya kukubali kipigo cha 4-1 mjini Lubumbashi.
You must be logged in to post a comment.